JWTZ yazungumzia habari iliyochapishwa na DIRA "Kifaru cha kivita cha JWTZ chaibwa"
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limekanusha taarifa za kuibwa kwa kifaru chake kwa kusema kuwa taarifa hizo si za kweli na kusisitiza kuwa ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara.
Hata hivyo Jeshi hilo limelitaka Gazeti la Dira kuomba radhi mara moja lasivyo hatua kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.