Taarifa iliyotolewa na chama cha ACT-Wazalendo kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hichoAnne Mghwira imesema kwamba kongamano hilo lililenga kumpa fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika hali isiyo ya kawaida walipewa taarifa na mwenye ukumbi (LAPF Millenium Tower) kwamba polisi walikuwa wametanda katika eneo la ukumbi tangu saa kumi mbili asubuhi na ilipofika saa nne kamili asubuhi mwenye ukumbi aliwataarifu rasmi kuwa amepewa taarifa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni kwamba chama chao hakina kibali cha kufanya kongamano hilo na hivyo asiwafungulie ukumbi huo.
Hivyo kupitia taarifa hiyo chama ACT-Wazalendo kimesema kimesikitishwa sana na hatua hiyo ya polisi na wanaitafsri kuwa ni mwendelezo wa hatua za uhakika katika kufifisha demokrasia katika nchi.
MAPITITIO YA BAJETI YA 2016/17 KWA MTAZAMO WA KIZALENDO
Chama cha ACT-Wazalendo kinawaalika kushiriki katika Semina ya Uchambuzi wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2016/2017. Katika Semina hii, tutachambua Bajeti iliyowasilishwa na Serikali Bungeni Pamoja na Kuainisha Njia Mbadala za Kuhakikisha Bajeti hii inalenga kuchochea Ukuaji wa Uchumi Shirikishi na Ustawi wa Jamii kwa Kuzingatia Misingi ya Usawa, Uwajibikaji, Demokrasia na Uongozi Bora.
Dhana kuu itakayoongoza Uchambuzi ni Ujenzi wa Taifa lenye Kujitegemea kwa kuzingatia Misingi ya Ujamaa wa kiDemokrasia.
Siku: Kesho, Jumapili, 12 Juni 2016
Muda: Kuanzia Saa 7 Mchana - 11 Jioni
Ukumbi: Millenium Towers, Kijitonyama, Dar es Salaam
Mzunguzaji Mkuu: Ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (MB), Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo
Wachangiaji Wengine Ni:
Wote Mnakaribishwa
- Prof. Kitila Mkumbo
- Ndugu Anna Mghwira
- Ndugu Godphrey Mwang'onda
TAARIFA KWA UMMA
Tunaujulisha UMMA kwamba Kiongozi wa Chama chetu cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe amekuwa anatafutwa na Polisi tangu jana usiku.
Mpaka sasa hatujui Kiongozi wetu yupo wapi na yupo kwenye Hali gani. Askari kanzu wanalinda nyumbani kwake na kwa watu wake wa karibu.
Sisi kama chama tunaliambia jeshi la Polisi kuwa lolote litakalotokea kwa Kiongozi wetu wao watajibu kwa umma.
Msafiri Mtemelwa,
Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo