Loading...
Saturday

Kauli ya Jumuiya ya Watanzania waishio kaskazini mwa California kuhusu Balozi

JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHERN

CALIFORNIA (TCO) JUNE 3 2016 TAMKO RASMI


Jumuiya yetu ya watanzania tuishio upande wa northern California,

Tunapenda kutoa tamko rasmi kwamba hatuhusiki na wala hatujahusishwa na hatutahusika kwa njia yoyote ile kushiriki kuweka sahihi zetu kwenye barua inayosemakana ipo na inahitaji sahihi za watanzania wanaoishi hapa ili kumlazimisha au kumshinikiza Rais amuondoe Mh Balozi Masilingi.

Habari hizi zilitolewa juzi kwenye vikao vya bunge na Mh Joseph Mbilinyi alipokuwa akichangia kwenye hotuba ya waziri wa mambo ya nje. Pamoja na mengi mazuri aliyoyasema kuhusu diaspora lakini hili la kuishambulia ofisi ya ubalozi kutoshiriki na kutojali misiba ya watanzania wanaoishi USA, sio tamko letu sisi wanajumuiya na hatuhusuani na lawama hizi. Pili hili la kutaka kumuondoa Balozi Masilingi kwa nguvu nalo hatuhusiki na hatutausika kamwe. Tunatambua mchango mkubwa na ushirikiano mkubwa tunaoupata kutoka ubalozini.

Tunapenda kutoa ukumbusho kuwa sisi kama jumuiya hatujihusishi na siasa kabisa. Tunajihusisha na masuala ya kijamii katika mazingira tunayoishi na pia nyumbani.
Tunatoa pongezi kwa makundi na jumuiya nyingine za hapa usa walioliona hili na kulikemea hadharani.

Lakini pia jumuiya yetu haimzuii mtanzania yeyote miongoni mwetu kushirikishwa kwenye shughuli yoyote ile, ilimradi tu aifanye kwa utashi wake lakini si kwa jumuiya.

Asante
Erick Byorwango - Katibu mwenezi na mahusiano TCO.
Nakala: Ofisi ya ubalozi Washington DC.
 
Toggle Footer
TOP