Kunguni hospitalini...


ZIARA ya kushtukiza ya Kamati ya Siasa ya CCM ya wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora katika hospitali ya wilaya hiyo, imeibua kitu kilichowaacha wengi midomo wazi. Kwamba katika wodi zake mbili, wamekutwa wadudu jamii ya chawa.

Kwa kiasi kikubwa, wadudu hao huishi kwa kufyonza damu na wana uwezo mkubwa wa kibaiolojia wa kujitengenezea kinga dhidi ya sumu kali. 

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Godfrey Mgongo alidaiwa kuwa katika wakati mgumu baada ya wadudu hao kubainika kusambaa katika wadi za hospitali hiyo, ikiwemo ya watoto.

Akijitetea mbele ya kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Costa Olomi na Katibu wake, Abdallah Kazwika, Mgongo alikiri kuwepo kwa kunguni wengi katika hospitali hiyo na kusema kuwa wamekuwa wakijitahidi kupuliza dawa, lakini kunguni wamekuwa wakijirudia mara kwa mara.

Aidha, Muuguzi Mkuu wa Wilaya, Shekha Ally alisema pamoja na juhudi zao za kupuliza dawa, dawa hiyo imekuwa haiui kunguni hao, ambapo kwa sasa wanatumia maji ya moto kwa kuyamwaga kwenye vitanda na magodoro.

Soma zaidi tahariri ya mhariri wa gazeti la HabariLeo