Mkuu wa Mkoa Dar afuta kibali na kusimamisha kampuni za ukandarasi

 photo ff-barabara-pg8-231112.jpg

SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam, imeifutia kibali kampuni ya Ukandarasi ya Ishinomya cha kufanya ujenzi wa barabara za halmshauri zote za jiji la Dar es Salaam kutokana kujenga barabara chini ya kiwango huku kampuni tatu zimetakiwa zisipewe zabuni mpaka pale watakapojiridhisha.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kampuni zimekuwa ukandarasi zimekuwa zikifanya kazi chini ya kiwango ili barabara iharibike kwa ajili ya kupata zabuni nyingine.

Amesema kuwa hatuwezi kufika kwakuwa na barabara zenye kiwango cha chini na kuendelea kuwepo kwa kampuni hizo ambazo zinajenga barabara chini ya kiwango na wanapofika mwisho nyuma zimeharibika.

Amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaam barabara zina mashimo kutokana na kampuni kufanya kazi kwa mazoea.

Kampuni ambazo zimesimamishwa kufanya ukandarasi wa barabara mpaka wajiridhishe ni Germinex, Delmonte pamoja na Skol.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam ndani ya mwezi mmoja kuwe hakuna barabara inayokuwa na mashimo na ni agizo ambalo wanatakiwa kutekeleza.
  • via Michuzi blog