Loading...
Monday

Mwanafunzi S/Msingi agoma kunywa dawa kwa hofu "ni ya Freemason"

Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Mapinduzi, wilyani hapa, Mkoa wa Mara. Rehema Samson amegoma kunywa dawa ya kinga inayotolewa bure kwa wanafunzi kwa ajili ya magonjwa yaliyosahaulika (kichocho na minyoo) kwa madai hajawahi kutumia dawa za hospitali toka azaliwe.

Baadhi ya wazazi inadaiwa wamewazua watoto wao wasipokee kinga hiyo inayotolewa bure na Serikali kwamba ni ya Freemason. Imani hiyo imekwamisha mpango huo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mapinduzi B’, Obwana Tom alikiri kuwa siku ambayo dawa hizo zilitolewa, mahudhurio ya wanafunzi yalishuka.
  • via gazeti la MWANANCHI

0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP