Mwang'onda, Kitomari speaks with CCTV about "Tanzania Budget 2016/17"


UFAFANUZI

Nimepokea jumbe nyingi zikielezea kuwa mimi nimetoa maelezo ya kufafanua jinsi ya tozo ya kwenye miamala ya simu zitakavyotozwa. Hayo maelezo yametolewa na ndugu Mtatiro, lakini napenda kukanusha kuwa lile andiko sio langu, inawezekana kuna mtu atakuwa amenitag then ndugu Mtatiro akahisi ni mimi ndie nilieandika.

Sasa labda nitoe ufafanuzi wangu kwa tozo hii, ni kwamba hakuna kodi yeyote inayotozwa kwasababu mtu anamiliki fedha either hizo fedha zipo benki au kwenye kibubu nyumbani kw ako, hizo fedha ni za kwako, hakuna kodi za style hiyo. Hii kodi ya 10% excise duty inatozwa kwenye income, mapato yanayotokana na miamala hii na sio fedha zilizotumwa au zinazotolewa kwenye simu.

Sote tunajua kuwa pale unapotuma fedha au unapotoa fedha kwenye simu kuna charges yani namaanisha kuna tozo tunazochajiwa na makampuni ya simu na mawakala nao huwa wanakuwa na commission yao pale. Sasa hii tozo ambayo makampuni ya simu yamekuwa yakitukata au yakituchaji wakati wa kutoa ilikuwa haikatwi kodi hii kabisa, kwa minajili hiyo basi serikali imeonelewa ni vyema sasa hili pato linalokwenda kwenye makampuni ya simu nalo likatozwa kodi kimsingi ni kwamba hili pato lilikuwa limesahaulika flani tu.

Kwahiyo hatutarajii mtumaji wa fedha ambaye ni mimi na wewe kukatwa hii kodi ila uwezekano wa hizi charges kuongezwa na makampuni ya simu ni mkubwa ili burden(mzigo) ya kulipa hii kodi imuangukie mlaji/mtumiaji wa huduma hii. Shifting of burden.

Nia ya hii kodi kodi ni kuhakikisha kila kamisheni inayotokana na miamala ya fedha kwenye simu inatozwa kodi. Hii kodi ilikuwa ikitozwa wakati wa kutuma fedha tu na si kutoa. Kwakuwa makampuni ya simu yanatoza pande zote wakati wa kutoa na wakati wa kutuma basi ndio maana halisi ya kutozwa kodi kwenye charges za nyakati zote za kutoa na kutuma

Nadhani nimeeleweka ndugu zangu, muwe na usiku mwema na ile kodi ya benki ni benki charges ndio inatozwa kodi sio fedha yako. Bank charges ni income kwa bank na ndio wameanzisha VAR kwenye hiyo income japo naona kutakuwa na changamoto kubwa katika kutekelezwa kwa hii kodi.

@GM
via Facebook