Polisi yakamata risasi 853 zilizofichwa kwenye gudulia


JESHI la Polisi mkoani Morogoro, limekamata risasi 853 zinazotumika kwenye silaha aina ya G3 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye dumu la lita 20 pembeni mwa mto Ngerengere eneo la Kihonda.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira ametoa taarifa kwa waandishi wa habari akisema risasi hizo zilikamatwa jana jioni eneo la Kihonda Kilimahewa.

Rwegasira amesema polisi wakiwa katika utekelezaji wa mapambano dhidi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kwa kufanya msako maeneo mbalimbali ndipo walipopata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna risasi zimehifadhiwa na watu wasiojulikana pembezoni mwa mto huo.
  • via GPL