Niko Chuo kikuu Mzumbe mwaka wa kwanza.
Nimetiwa moyo sana kupitia Radio hii hususani pale nilipokutana na Mtangazaji makini kabisa wa kituo hiki bora cha matangazo (JOHN MINJA),nilipokutana nae mara ya kwanza katika Usiku wa Patakatifu Pake pale CAG.
Ningependa kupata nafasi redioni hapo japo kutembelea tu na kuona namna ya urushwaji wa matangazo unavyoenda hapo studio.
Hii ni kwa sababu ninapenda sana utangazaji kutoka moyoni na ndio kipaji changu, hivyo naamini ipo siku nitafikia ndoto hii.
Ahsante!
D.R. (jina kamili na email address vimehifadhiwa)