Rasimu ya Katiba - The Federation of Tanzanians Communities/Associations in the UK and NI - TZUK

KAMATI YA MPITO – TZUK YAKAMILISHA RASIMU YA KATIBA, KUUNDA SHIRIKISHO LA JUMUIYA NCHINI UINGEREZA, RASIMU TAYARI IMEIVA KWA KUIDHINISHWA NA MKUTANO MKUU WA WATANZANIA WOTE WANAOISHI NCHINI UINGEREZA (UK & NI)


Salaam, Kwa niaba ya Kamati ya Mpito - TZUK naambatanisha Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na kamati hii chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wake Eng. Dr. Julius Hingira, Kamati hii, ilichachaguliwa na watanzania wenyewe mwishoni mwa mwezi April mwaka 2016, na kupewa muda wa siku tisini kukamilisha kazi yake. Kamati ilijitambulisha ubalozini na kupata kufahamika rasmi kama chombo kilichopendekezwa na watanzania wenyewe.

Rasimu hii imezingatia maoni ya watanzania wanaoishi hapa nchini Uingereza na kuandikwa katika mfumo unaokusudia kuleta umoja, mshikamano na upendo, wakati wa shida na furaha, kwa kuunganisha nguvu za Jumuiya zote zilizopo hapa UK na Northern Ireland na kutoa rai ya kuanzishwa kwa Jumuiya katika maeneo ambayo hakuna Jumuiya, yaani “local community”.

Pia Rasimu imejikita katika mazingira yanayozingatia kujiendeleza kiuchumi, ajira na uwekezaji, ushauri na kujishirikisha katika kuboresha sekta mbalimbali za umma na binafsi, bila kusahau usaidizi wa misaada mbalimbali nyumbani Tanzania, katika nyanja za elimu, afya, kilimo, etc na umiliki wa rasilimali kwa manufaa ya wanajumuiya.

Rasimu hii ya katiba itawakilishwa kupata baraka, katika mkutano mkuu wa pamoja kwa watanzania wote utakaondaliwa na ubalozi wetu hapo baadae kwa maagizo ya Mh. Waziri Mkuu alipozungumza nasi katika ziara yake hivi Karibuni.

Hivyo basi ni vyema tukaipitia kwa kusoma kipengele kwa kipengele na kuwafahamisha wengine kwa kuisambaza rasimu hii iwezekanavyo ili iwafikie watanzania walio wengi zaidi na tuweze kupata maoni yao zaidi kabla ya kuidhinishwa na mkutano mkuu wa pamoja na kupanga tarehe ya kufanya uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya kuu Shirikisho moja, itakayoundwa kwa uwakilishi wa Jumuiya za maeneo mbalimbali hapa UK na Northern Ireland.

Pia kamati ya Mpito itafanya kazi ya kuelimishana kuhusu rasimu hii na kubabadilishana mawazo na watanzania wote hapa UK, kwa kila aina ya mawasiliano ili kufanikisha zoezi hili kwa ufasaha.

Rasimu hii pia itapatikana katika mitandao mbalimbali online kama facebook, blogs, websites, whatsapp na telegram phone appilication za TZUK na nyingine nyingi za kitanzania etc.

Facebook ya TZUK ni: facebook.com/tzuk.diaspora, Twitter page ni twitter.com/TZUKDiaspora, website: tzuk.org.uk.

Rasimu ya Katiba link hii: https://files.acrobat.com/a/preview/def4a1a2-3041-45f1-a967-7b74a579dc72

Natanguliza shukurani, wenu katika ujenzi wa Jumuiya;

Abraham Sangiwa
...................................................