Loading...
Thursday

Shukurani za Bi. Janeth Magufuli kwa T.B. Joshua kwa msaada alioutuma kwa ajili ya wazee Mtwara

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Kiongozi wa Wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka Bw. Boniface Mbedo misaada leo Mkoani Mtwara.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Baadhi ya viongozi wa serikali, chama na wazee wakati akiwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka kwa ajili ya kutoa misaada ya chakula, mavazi pamoja na vifaa vya malazi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara kwa ajili ya kutoa misaada ya chakula, mavazi, madawa pamoja na vifaa vya malazi.
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara
Baadhi ya Wazee walimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Bw. Rashidi Kambona akimkabidhi taarifa ya kituo hicho mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wazee katika kituo cha Nkaseka Mkoani Mtwara na kumshukuru mtumishi wa Mungu TB Joshua kuunga mkono juhudi zake za kuwasaidia wazee na watu wasiojiweza kwa kuchangia baadhi ya vitu vilivyotolewa kama msaada kwenye kituo hicho.
Muwakilishi wa Mtumishi wa Mungu TB Joshua Nchini Tanzania akitoa salamu kutoka kwa TB Mhandisi Consolata Ngimbwa Joshua aliyetoa msaada kwa ajili ya wazee wa kituo cha Nkaseka kilichopo Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo na moja ya Mzee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka baada ya kumpa zawadi ya Ungo, Chungu na Mwiko. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa, wakati wa hafla ya utoaji misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Nkaseka Mkoani Mtwara.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wazee wa kituo cha kulea wazee cha Nkaseka kilichopo Mkoani Mtwara.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (Kushoto) na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa wakimsalimia moja ya mzee katika kituo cha kulea wazee cha Nkaseka kilichopo Mkoani Mtwara.

0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP