Taarifa ya polisi ya kukamilika kwa zoezi la kuhakiki silaha na kuanza operesheni kwa wasiohakiki

Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato M. Mssanzya – CP
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu zangu waandishi wa habari,

Leo tarehe 30.6.2016 ndiyo tarehe na siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha. Kwa mujibu wa takwimu za silaha tulizonazo inaonyesha kwamba wapo baadhi ya wamiliki wa silaha ambao hawajatekeleza agizo la kuhakiki silaha wanazozimiliki.

Kufutia hali hiyo, natoa angalizo kwa wale wote ambao hawajahikiki silaha zao kwamba muda wowote kuanzia sasa tutaanza operesheni maalum ya kutafuta silaha ambazo hazijahikikiwa. Ifahamike kwamba yeyote atakaye kutwa na silaha ambayo haijahakikiwa atachuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupoteza sifa ya kuwa mmiliki halali wa silaha hiyo.

Tunatoa agizo kwa wamiliki binafsi wa maghala ya silaha waziwasilishe silaha hizo pamoja na nyaraka zake katika vituo vya karibu vya Polisi kwa ajili ya uhakiki.

Imetolewa:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo

Makao Makuu ya Polisi