Taarifa ya TRA ya tarehe ya mwisho ya kulipa Kodi ya Mapato na ya Ongezeko la Thamani

ISO 9001:2008 CERTIFIED

Walipakodi wote wanakumbushwa kuzingatia mwisho wa kulipa kodi ya Mapato na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) PASIPO ADHABU

1.O ULIPAJI WA KODI YA MAPATO – MAKADIRIO YA AWALI
  • walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/06/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya nne ya makadirio ya awali ya mwaka 2016
  • walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/09/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya tatu ya makadirio ya awali ya mwaka 2016
  • walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/12/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya pili
  • walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 31/03/2017, wanapaswa kulipa sehemu ya kwanza ya makadirio ya awali ya mwaka 2017
Tarehe za malipo kwa ufupi:

Tarehe ya mwisho wa mwaka wa Mahesabu Awamu za Malipo Tarehe ya Mwisho wa Malipo bila Adhabu

30/06/2016 Awamu ya nne ya mwaka wa Mapato 2016 30/06/2016
30/09/2016 Awamu ya tatu ya mwaka wa Mapato 2016 30/06/2016
31/12/2016 Awamu ya piliya mwaka wa Mapato 2016 30/06/2016
31/03/2017 Awamu ya kwanza ya mwaka wa Mapato 2017 30/06/2016

2.0 UWASILISHAJI WA RITANI ZA MAPATO KWA MWAKA 2016

Walipakodi wote ambao mwaka wao wa mapato uliisha tarehe 31/12/2015, wanatakiwa kuwasilisha ritani zao pamoja na hesabu zilizokaguliwa na kulipa kodi yote inayotakiwa mnamo au kabla ya tarehe 30/06/2016

3.0 UWASILISHAJI WA RITANI ZA VAT ZA MWEZI MEI 2016

Walipakodi wote ambao wamesajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wanatakiwa kuwasilisha ritani za mwezi mei 2016 na kulipa kodi inayotakiwa kabla ya tarehe 30/06/2016. Pia wale wote ambao hawakufanya biashara wanatakiwa kuwasilisha ritani zao zisizokuwa na malipo (NIL RETURN)

4.0 UTOAJI WA RISITI ZA KODI ZA KIELEKITRONIKI/ ANKARA YA KODI 

Walipakodi wote waliosajiliwa na wasiosajiliwa kwenye kodi ya Ongezeko la Thamani wanakumbushwa Kutoa risiti za kodi za kielekitroniki/Ankara ya kodi kwa mauzo yote wanayofanya kulingana na fedha zilizopokelewa. Ni kinyume cha sheria kupokea malipo kwa kuuza Bidhaa au huduma bila Kutoa risiti ya kodi ya kielekitroniki/Ankara ya kodi

5.0 KUMBUKA

Riba na Adhabu itatozwa/itatolewa kwa Pointi ya Sarafu (Currency Points) kwa mlipakodi yeyote ambaye hatalipa kodi kwa muda unaotakiwa au atakayeshindwa kuwasilisha ritani kwa muda unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Ili kuepuka msongamano na usumbufu mwingine walipakodi wanashauriwa kutosubiri siku ya Mwisho. Tunashukuru kwa ushirikiano mzuri.

“Pamoja Tunajenga taifa letu”

Imetolewa na:

Idara ya Huduma na Elimu kwa mlipakodi
TRA Makao Makuu
S.L.P 11491
Dar es Salaam.

Barua pepe: [email protected]

Kituo cha Huduma
Simu bila Malipo
0800 780078
0800 750075