Taarifa ya uteuzi wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF

Uteuzi Wa Bodi Ya Wadhamini Wa Shirika La Taifa La Hifadhi Ya Jamii (NSSF) 

Ofisi ya Waziri Mkuu inapenda kuutaarifu umma kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Prof. Samwel Mwita Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuanzia tarehe tarehe 30 Mei, 2016 kwa kipindi cha miaka mitatu.
Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake katika Sheria ya Msimamizi na Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Na.5/2012. (The Social Security Laws (Amendements) Act.2012 jedwali la pili (Second Schedule) kifungu cha 2 (1).

Aidha, kwa mujibu wa Sheria hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb.) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
  1. Bw. Paul Daud Sangize – Mwakilishi wa Wafanyakazi
  2. Bw. Noel Nchimbi – Mwakilishi wa Wafanyakazi
  3. Bw. David Magese – Mwakilishi wa Waajiri
  4. Bibi Margreth Chacha – Mwakilishi wa Waajiri
  5. Bw. Justine Mwandu – Mwakilishi wa Sekta Binafsi
  6. Bw. Gabriel Pascal Malata – Mwakilishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
  7. Bw. Emmanuel Maduhu Subi – Mwakilishi wa Wizara ya Fedha na Mipango
  8. Bw. Ally Ahmed Msaki – Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Eric F. Shitindi

KATIBU MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
DAR ES SALAAM