Ike ambaye alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), Mei 11,2013, amehukumiwa adhabu hiyo jana na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Benedict Mingwa.
Jaji Mingwa amesema upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili mwandamizi wa Serikali, Tamari Mndeme, umeithibitishia mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Awali, Tamari akisaidiana na mawakili wenzake waandamizi,Saraji Iboru na Jullius Semali, alidai mshtakiwa alikuwa anataka kusafirisha dawa hizo zenye thamani ya Sh313.6 milioni kwenda Burkina Faso.
************************
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi imemhukumu kifungo cha maisha gerezani raia wa Togo, Josiane Dede (25) kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya shilingi 116/= milioni.Akitoa hukumu hiyo juzi, Jaji wa Mahakama hiyo, Benedict Mwingwa alisema imeridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande wa mashtaka.
Alisema kutokana na ushahidi huo, Mahakama inamtia hatiani mshtakiwa huyo kwa kosa la kusafirisha dawa hizo zenye uzito wa gramu 1,989 kinyume cha Sheria namba 6 kifungu cha 31 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
Jaji Mwingwa alisema mwaka 2013, mshtakiwa huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na mabegi mawili, moja likiwa na dawa hizo.
Akitoa utetezi kabla ya hukumu kutolewa, wakili wake, David Shiratu alidai kuwa mteja wake anaiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kwa sababu ni mwanafunzi wa utalii katika Chuo Kikuu cha Togo na familia yake pamoja na nchi yake inamtegemea.
************************
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya imemhukumu kifungo cha miaka 25 jela na kulipa faini ya Sh3.19 bilioni raia wa Afrika Kusini, Vuyo Jack, baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 42.5.
Pia, Mahakama hiyo imeamuru kutaifishwa kwa gari lenye namba za usajili CA-508-650 aina ya Nissan lililokuwa likiendeshwa na raia huyo ambalo lilikutwa na dawa hizo na fedha zitakazopatikana zitaingizwa kwenye mfuko wa Serikali.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Noel Chocha alisema korti imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kwamba, adhabu hiyo itaanza kuhesabiwa tangu siku aliyokamatwa raia huyo Novemba 18, 2010.
Awali, akitoa maelezo katika hukumu hiyo ambayo ilichukua zaidi ya saa nne, Jaji Chocha alisema baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa katika mpaka wa Tunduma, kamati ya ulinzi na usalama ikiwa na ofisa wa kuzuia dawa za kulevya ilifanya ukaguzi wa gari hilo na kukuta paketi za dawa hizo zilizokuwa zimewekwa maeneo mbalimbali na kwenye chasesi.
Alisema baada ya ukaguzi huo ulifanyika uchunguzi wa awali kupitia mtaalamu wa dawa za kulevya chini ya kamati hiyo na kuzikuta zikiwa na uzito huo.
Mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali, Joseph Pande akisaidiana na Rogers Francis aliieleza Mahakama kuwa hakuna kumbukumbu inayoonyesha mtuhumiwa aliwahi kutenda kosa kama hilo, lakini aliiomba itoe adhabu kali.
Akitoa utetezi, wakili wa kujitegemea aliyeombwa na Mahakama hiyo kumtetea raia huyo, Ladislaus Lweikaza aliiomba kumpunguzia adhabu kutokana na kukaa miaka sita gerezani akiwa mahabusu.
- via MWANANCHI