Ufafanuzi kuhusu kujitoa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU KUJITOA KWENYE MIFIKO YA HIFADHI YA JAMII

Siku za hivi karibuni kumekuwa na mkanganyiko wa taarifa zisizo rasmi kuhusu kusitishwa KUJITOA KWENYE MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

Mamlaka inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

Kila Mfuko wa Hifadhi ya Jamii unaongozwa na sheria yake iliyopitishwa na Bunge. Kama mtakavyokmbuka, Mwaka 2012 Serikali ilifanya marekebisho ya Sheria za Mifuko ya HIfdhi ya Jamii kupitia Sheria Na.5 ya Mwak 2012. Lengo la marekebisho hatyo ilikuwa kuhuisha Sheria hizo. Hata hivyo, iligundulika kuwa marekebisho hayo hayakugusa vipengele vya baadhi ya Mifuko.

Hali hii ililazimu Serikali kuahidi Bunge kwamba, itapitia upya sheria hizo hasa kipengele cha kujitoa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

HIvyo Mamlaka inapenda kuwajuilsha kwamba, Serikali ipo katika hatua nzuri za kuandaa marekebisho madogo ya Sheria ili kuhuisha Sheria zote ikiwa ni pamoja na kulipatia ufumbuzi aw kudumu suala la kujitoa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Kwa sasa Mamlaka inawaomba Wanachama wote waendelee kuwa na utulivu wakati Serikali ikiendelea kulifanyia kazi suala hilo.

Imetolewa na 

Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P. 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz 
Dar es Salaam