UKAWA watoka Bungeni kwa mabango yenye jumbeWABUNGE wa Kambi Rasmi ya Upinzani leo asubuhi wameingia bungeni wakiwa wamevalia nguo nyeusi wote walipohudhuria kikao cha 54 cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma.

Baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson kuingia bungeni na kuongoza dua ya kuliombea Bunge, walianza kunyanyua mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakitoka nje ya ukumbi wa bunge hilo.

Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma mara baada ya kutoka nje, Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, James Mbatia, amesema hawajatoka wala kulikimbia bunge, na kwamba wapo bungeni na wanaendelea kufanya kazi za bunge.
“Hatujakimbia bungeni, tunashiriki kwenye kamati, hatujasusia bunge, tumechukizwa, tunahasira na vitendo vya kibabe, vya kionevo vinavyofanywa na kiti.” Alisema Mbatia