Upinzani Tanzania waziba midomo kwa karatasi na gundi na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma.

WABUNGE wa Kambi ya rasmi ya Upinzani Bungeni, leo wameibuka na mtindo wa aina yake ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodoma, baada ya kuamua kuziba midomo yao kwa kugundisha karatasi na plasta kisha kutoka nje ya ukumbi huo ikiwa ni adhima ya kueleza hisia zao za kutosikilizwa mapendekezo yao na Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
Hali ya wabunge wa Kambi ya Upinzani walianza kutoka nje ya bunge hilo yapata wiki ya pili mfululizo kutokana na kile walichokitangaza kuwa, hawatahudhuria kikao chochote cha bunge hilo kitakachoongozwa na Naibu Spika Dkt. Tulia kwa kuwa amekuwa akiwanyima wapinzani nafasi ya kutoa maoni yao bungeni hivyo kuminya haki yao ya msingi ya ikiwa wao ni wawakilishi wa wananchi.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kusikiliza hoja na mapendekezo yao ndani ya bunge hilo.

Nje ya Bunge
Wabunge wa Upinzani wakiziba midomo yao.


Wakitoka nje ya ukumbi wa bunge hilo.