[video] Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa makabidhiano ripoti ya Uchaguzi Mkuu 2015


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Ikulu, kwa ajili ya makabidhiano ya taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya Makabidhiano ya taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015.

Taarifa hiyo imekabidhiwa leo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Damian Lubuva kwa Mhe. Rais Magufuli, katika hafla iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wastaafu wa Serikali, Viongozi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar, Waheshimiwa Mawaziri na Viongozi Waandamizi wa Serikali, wengine ni Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaowakilisha nchini.

Mhe. Rais akionyesha taarifa aliyokabidhiwa na Mhe. Lubuva kwa wageni waalikwa

Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijadili jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi(Katikati) mara baada ya kuwasili Ikulu kwaajili ya kushuhudia makabidhiano hayo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima (wa kwanza kulia) akifuatilia hotuba iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Rais Magufuli

Mkuu wa Mabalozi, Mhe. Ambrosio Montecilo Balozi wa Angola nchini (wa kwanza kushoto) pamoja na Mabalozi wengine wanaowakilisha mataifa yao nchini wakishuhudia zoezi la makabidhiano ya taarifa ya NEC

Sehemu nyingine ya Mabalozi wakishudia makabidhiano

Kaimu Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. James Bwana (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa wakiratibu hafla hiyo.

Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Wakuu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar, Viongozi wengine Wakuu wa Serikali na Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mhe. Rais na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Serikali

Mhe. Rais na meza kuu katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaowakilisha hapa nchini

Mhe. Rais na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)

Bw. James Bwana akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo

Waziri Mahiga akijadili jambo na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.