[video] Kauli ya Sumaye na Polisi walivyowatawanya wanafunzi waliokuwa kwenye mahafali Dodoma


Video iliyopachikwa hapo chini inaonesha ilivyotokea leo katika ukumbi wa hoteli ya African Dream mjini Dodoma, ambapo jeshi la polisi limewatawanya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa katika ukumbi huo kwa ajili ya kushiriki mahafali yaliyoandaliwa na viongozi wa chama hicho.


Inayovuata ni video ya wanafunzi wa vyuo vikuu Dodoma waliozungumza na waandishi wa habari mara baada ya polisi kuwatawanya katika hoteli ya African Dream.


Ya mwisho ni video ya alichokisema Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye leo, katika ukumbi wa hoteli ya African Dream mjini Dodoma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya jeshi la polisi kuwatawanya wanafunzi wa vyuo vikuu waliokuwa kwenye mahafali.