Wabunge wahoji adhabu na utekelezaji wake kwa aliyehukumiwa kumdhihaki Rais Magufuli

Habari ya kufikishwa mahakamani (bofya hapa) na kuhusu hukumu (bofya hapa) kisha endelea...

Juni 9, 2016 via MWANANCHI -- Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.

Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.

Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (CHADEMA), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh 800,000/- ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.

Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.
"Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema.


Juni 18, 2016 via MWANANCHI -- Wanaharakati na wadau wa mitandao ya kijamii nchini wamemkabidhi Sh4.5 milioni aliyekutwa na hatia ya kumtukana Rais John Magufuli ili akaulipa faini aliyotakiwa atoe na mahakamani kuepuka kifungo cha miaka mitatu.

Mshtakiwa huyo, Isaack Habakuki alikutwa na hatia baada ya kukiri kosa la kumtukana Rais kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imemtaka kutoa Sh 7 milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Mratibu aliyekuwa anakusanya michango hiyo kwa Kanda ya Kaskazini, Diwani wa Levolosi, Ephata Nanyaro amesema jana kuwa wamefanikiwa kupata michango hiyo kupitia makundi ya mitandao ya kijamii waliyoyaanzisha.
"Lengo ni kumsaidia mwenzetu kwa kuwa kupitia sheria hii ya mitandao tunaamini hakuna aliyesalama na sheria hii itawagusa wote, " amesema Nanyaro.
Naye, Habakuki amewashukuru Watanzania waliojitolea kumchangia akisema kupitia adhabu hiyo atakuwa wa kwanza kufundisha jamii kuhusu sheria za mitandaoni