Ulimwengu amesema ni kutokana na kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ulimwengu amesema katika hili hamna kifimbo cha uchawi cha kujinasua isipokuwa mchakato wa katiba ambao ulichukua fedha nyingi kisha ukaachwa njiani na Mheshimiwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Ulimwengu ameendelea kwa kusema Mheshimiwa Kikwete anatakiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka kwa kusababisha hasara kubwa kwa serikali na pili kuzima matumaini ya wananchi na kuwaacha wanarandaranda ambayo inaweza kuleta machafuko baadaye kama haitawezekana kutengeneza katiba ambayo itajenga mustakabali wa wananchi wa Tanzania.
Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ameongea kwenye Kongamano la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kuongelea nyufa zilizopo na kusema ni kutokana kupenda kuzungumza watu badala ya sera.
Mkapa pia amegusia kuhusu kizazi kipya na amewataka watu kufatilia michango ya vijana bungeni ambao hawajafanya kazi hata miaka mitatu, uchambuzi na mbadala gani wanapeleka bungeni na kusema hapana kwenye kulalamika.
Mkapa amesema anakubali kuwa kiongozi ni lazima aweze kusikiliza na ilikuwa ni sifa mojawapo ya Mwalimu lakini watu ni hodari wa kusema nini kifanywe mpaka inafika wakati unatokea umuhimu wa kunyamazisha.
"sasa umuhimu wa kukunyamazisha wewe lazima tuutafakari, maana mara nyingine unatu-distract from the issues."
On Freedom of Expression, "...Ngoja niwaambieni basi, mimi ndiye niliyemwambia Aga Khan, njoo anzisha magazeti mengine hapa. Ya serikali na IPP hayatoshi pake yake. Nataka ku-broaden perspective, ndiyo maana ikaja kampuni ya Mwananchi na kuanzishwa kwa Citizen na Mwanchi, at my request! That's the kind of intolerance I have."