Waziri, Prof. Muhongo alivyoadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa

Leo tarehe 25 June 2016 ni siku ya kuzaliwa ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo.

Katika sherehe yake ya kuzaliwa, Profesa amefanya yafuatayo:
  1. Amewakaribisha Madaktari Mabingwa kutoka China kutoa matibabu na dawa bure kwa wanavijiji kwa siku mbili.
  2. Amegawa zaidi ya vitabu 22,000 kutoka Marekani (thamani: US $ 250,000), sawa na TSh 500 milioni, kwenye shule za msingi 108 na sekondari 20.
  3. Kupata birthday lunch ya ugali na sato kijijini Kigera. 
  4. Kesho atagawa madawati 1,812. 
Hiyo ndiyo birthday ya Mbunge wetu Mhe. Prof. Sospeter Muhongo.

Mungu amuongezee miaka mingi ili awatumikie wananchi na kuinua maisha ya wanyonge wa nchi yetu.