CDA yatimua wapangaji ili ikarabati nyumba


Wakazi zaidi ya 100 leo wameondolewa kwa nguvu katika nyumba zinazomilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) baada ya kukaidi agizo la kuhama kwa hiari ili kupisha ukarabati.

Wamiliki hao waliondolewa na kampuni ya udalali ya Mvina, zoezi liloanza asubuhi leo chini ya usimamizi wa polisi waliokuwa na mabomu ya machozi na bunduki.

Awali wapangaji hao walipewa notisi ya kuhama kwa hiari ya siku 90 lakini baadaye wakaongezewa wiki moja iliyoisha leo.

Taarifa zinasema kuwa wapangaji ambao hawakuwepo wakati zoezi likiendelea, nyumba zao zilivunjwa milango na vifaa vyao kutolewa nje.

Baadhi ya wapangaji hao ambao hulipa kodi ya kati ya Sh 18,000 hadi 22,000 kwa mwezi kwa nyumba ya nyumba vitatu wanadaiwa madeni ya zaidi ya Sh 7 milioni.

Kwa mujibu wa CDA baada ya kukarabati huo wapangaji watakaokubali kuendelea kukaa katika nyumba hizo wataingia mkataba upya wa kupanga.