Chini ya mti huu, ndipo darasani...


Wakazi wa kitongoji cha Enderema kijiji cha Milughwe wilaya ya Longido wameomba serikali na wadau wa elimu kusaidia ujenzi wa darasa la awali ambalo wanafunzi wake wanasomea chini ya mti kwenye vumbi na jua kali tena katikati ya pori hali inayotishia watoto kupata magonjwa kama ya kufua kikuu na mengineyo.