Gugu Zulu, mwendesha magari ya langalanga Afrika Kusini afariki akikamlisha Trek4Mandela mlima Kilimanjaro

Raia wa Afrika Kusini waliopanda Mlima hivi karibuni kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua taulo za kusaidia watoto wa kike. Aliyechuchumaa mbele (mwenye kofia), Gugu Zulu ndiye anatajwa kufariki Dunia wakati akielekea Kileleni.
Na Dixon Busagaga 


Ra ia wa Afrika ya Kusini Guguleth Mathebula Zulu (38) aliyefika nchini kwa ajili utalii wa kupanda Mlima Kilimanjaro amefariki leo tarehe 18.7.2016 baada ya kupatwa na tatizo la kushindwa kupumua kwenye mwinuko wa juu mlimani.

Shirika la Hifadhi za Taifa nchini kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za serikali zinaendelea na uratibu wa kurejesha mwili wa marehemu nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya taratibu za maziko.

Zulu alifika nchini na kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro tarehe 14.7.2016 kwa ajili ya kuenzi jitihada za Rais wa Kwanza wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela za kusaidia familia maskini nchini Afrika ya Kusini, hususani kuwapatia mahitaji muhimu watoto wa kike ambao hawana uwezo wa kupata mahitaji muhimu.

Hii ni mara ya pili kwa watalii kutoka Afrika ya Kusini kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuenzi juhudi za Mandela katika kusaidia jamii ya watoto wa kike kupitia kampeni maalum ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

Imetolewa na 
Idara ya Mawasiliano Hifadhi za Taifa Tanzania
S.L.P 3134 
 
Baruapepe: [email protected] 
Wavuti: www.tanzaniaparks.go.tz
18.07.201


Gugu Zule (Kulia) akiwa na Richard Mabaso muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Gugu Zulu akiwa katika lango la Marangu akipata picha na mmoja wa washiriki wa safari hiyo muda mfupi kabla ya kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro.

Gugu Zulu (kushoto) akiwa na rafiki yake muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro katika kampeni ijulikanayo kama Trek4Mandela ikiwa na lengo la kchangisha fedha kwa ajili ya kunua taulo za watoto wa kike pamoja na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba wa taifa la Afrika Kusini ,Nelson Mandela.