Hatari hii! Wanatumia maji yanayochuruzika kutoka kiwanda cha mkonge
Wakazi zaidi ya 3,500 wa kijiji cha Mwenga kilichopo kata ya Mswaha wilayani Korogwe wanalazimika kutumia maji yanayodaiwa kuwa na kemikali zenye sumu yanayotoka katika mashine za kusindika Mkonge kufuatia mradi wa maji wenye thanmiani ya zaidi ya shilingi milioni 600 unaofadhiliwa na Benki ya Dunia uliotakiwa kukamilika miaka 2 iliyopita kushindwa kuendelea kwa sababu ya kujengwa chini ya kiwango.