Jana katika Baraza la Idi el Fitri lililofanyika katika ukumbi wa Wakfii wa Ngazija mjini Zanzibar, Katibu Mkuu wa chama cha Civic United Front (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema anasikitishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi mbalimbali wa chama hicho katika ngazi za wilaya na majimbo.
Amedai kuwa viongozi hao huwekwa ndani huku wakiteswa, kuadhibiwa na kulazimishwa kukubali kushiriki katika vitendo vya uhalifu ambavyo hawakuvitenda.
Hata hivyo, amesema kuna mwendelezo wa kauli zinazoashiria azma ya kutaka kumkamata yeye, zinazotolewa na baadhi ya wakuu wa vyombo vya dola na hivyo kutamka; “Hakuna haja ya kuwatesa watu, iwapo wanayo azma ya kunikamata, mimi nipo waje tu wanikamate.”