Hotuba ya Rais Mafufuli katika Baraza la Idi el Fitr 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikhe Aboubakar Zubeir wakati alipowasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la Eid El fitri lililofanyika katika viwanja hivyo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote na kupanua uwigo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za kijamii na ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 06 Julai, 2016 wakati akihutubia Baraza la Eid el-Fitr kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililofanyika kitaifa katika viwanja vya Karimejee Jijini Dar es salaam.

Dkt. Magufuli amesema kitendo cha kuwaunganisha waislamu wote katika Baraza la Eid el-Fitr kinafungua ukurasa mpya na ni moja ya hatua muhimu za kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu wa makundi mbalimbali pamoja na watanzania wengine waisio waislamu.

Aidha Rais Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha taasisi zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema serikali itahakikisha mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba wote waliodhulumu mali za waislamu watazirejesha.

Awali akisoma taarifa, Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaji Suleiman Said Lolila amesema BAKWATA inakusudia kupanua huduma za kijamii kwa lengo la kuwahudumia wananchi ikiwemo kujenga chuo kikuu Mkoani Dodoma na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuondoa umasikini huku akimtaka asikatishwe tamaa na wachache watakaoudhika kwa kuguswa na hatua zinazochukuliwa.

Nae Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kwa kuongoza bila ubaguzi amewataka watanzania kuungana na juhudi za serikali kupinga matendo maovu ikiwemo rushwa na ufisadi na pia amelaani ndoa za jinsia moja akisema ni kinyume na maadili ya dini.

Baraza la Eid el-Fitr pia limehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, mabalozi na wabunge.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
06 Julai, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la Eid Elfitri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir pamoja na Waziri Mkuu Kassim majaliwa wakati walipokuwa wakisiliza ujumbe wa Kaswida katika baraza la Eid Elfitri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Baraza la Eid Elfitri.

Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir akimshukuru Rais Dkt. Magufuli mara baada ya kuhutubia katika Baraza hilo.

Waumini wa dini ya kiislamu wakifatilia kaswida iliyokuwa ikiimbwa katika viwanja hivyo vya Karimjee.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika baraza hilo la Eid Elfitri.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wakifatilia hotuba hiyo ya mgeni rasmi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akaiomba dua pamoja na Mufti Mkuu Sheikhe Aboubakar Zubeir.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu mara baada ya kumaliza kuhutubia katika viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na mtoto Asma Maulid baada ya kuhubia Baraza la Iddi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria Baraza la Iddi alilolihutubia kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Julai 6,2016

  • PICHA NA IKULU