IGP vs Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi


NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusuf Masauni, ameingia katika mgogoro kwa kuingilia majukumu ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), anaandika Josephat Isango via MwanaHALISI Online.

Masauni anatuhumiwa kuingilia madaraka ya IGP kwa kuamuru Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, Mukadam Khamis Mukadam “kuondolewa” kwenye nafasi yake.

Hata hivyo, sikuchachebaadayauamuzihuo, IGP Ernest Mangu anadaiwa kuandika barua kuamuru Mukadam abaki kwenye nafasi yake.

Gazeti hili (MwanaHALISI) limeona barua mbili; moja ya kumuondoa Mukadam na nyingine ya IGP Mangu ya kumbakiza Mukadam kwenye nafasi yake.

Taratibu za jeshi la polisi zinaeleza kuwa mwenye mamlaka ya kuhamisha, kuonyana au kufukuza viongozi wajuu wa jeshi hilo ni IGP.

Taarifa zinaeleza kuwa RPC alitoa amri ya kukamatwa, kuhojiwa na kufikishwa mahakamani, dereva mmoja (jina tunalo) anayetuhumiwa kukaidi amri ya kusimama iliyotolewa na askariwa usalama barabarani. Dereva huyo anadaiwa kuwa na uhusiano na waziri Masauni. Badala ya kusimama, dereva huyo “alielekeza gari lake kwa askari wa usalama barabarani akitaka kumgonga,” polisi wameeleza.