John Mafuguli akabidhiwa, apokea kiti na kushika hatamu za uongozi wa Chama Cha Mapinduzi

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete akimkabidhi moja ya vitendea kazi, Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Dk. John Magufuli baada ua Wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM, kumpitisha asilimia kwa mia ya kura, katika kumchagua leo katika ukumbi wa Dodoma.
Mweneyekiti wa CCM mstaafu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mwenyekiti Mpya wa CCM Rais Dk. John Magufuli wakipunga mkono baada ya Magufuli kutawazwa rasmi kushika nafasi hiyo leo mjini Dodoma

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimpongeza Mwenyekiti mpya wa CCM Rais Dk. John Magufuli baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM kumchagua kwa kura asilimia mia kwa mia.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein akimpongeza Rais Dk John Magufuli baada ya kutawazwa rasmi kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM lo mjini Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete


Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akitoa hotuba yake, baada ya kutawazwa kushika nafasi hiyo kwa kupata kuta asilimia mia kwa mia zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM uliofanyika leo mjini Dodoma,.
  • Picha tumeshirikishwa na Bashir Nkoromo


Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kulia), akiwa pamoja na Diwani wa Kata ya Igoma Jijini Mwanza, wakiwa katika Viunga vya Ukumbi mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Dodoma wa Dodoma Convetional Centre ambapo Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unafanyika.

Ni Mkutano Maalumu kwa ajili ya Wajumbe hao kumchagua Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa, ambapo jana Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM walipitisha kwa kura zote jina la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa chama hicho. Dkt. Magufuli anapokea kijiti cha uongozi wa chama kutoka kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mji wa Dodoma umegubikwa na shamra shamra mitaa yote na tayari wajumbe wa Mkutano Mkuu wameanza kuingia Ukumbini kwa ajili ya Mkutano huo huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa vyema kila kona.


Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akisalimiana na mjumbe mwenzake wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma hii leo


Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (kushoto) akiwa na Katibu wake, Heri James, Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma hii leo


Heri James (kushoto) akiwa na mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, wakisalimiana ukumbini.


Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (kushoto), akiwa ukumbini na mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM.


Kaimu Katibu wa CCM mkoani Mwanza Elias Mpanda (kulia) akisalimiana na aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Manju Msambya (kushoto).


Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka mkoani Mwanza


Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM akiwemo Le Mutuz (kulia) wakiperuzi taarifa mbalimbali kuhusiana na Mkutano huo.


Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akitoa burudani na Bendi ya TOT Pus


Ni burudani kutoka kwa bendi ya TOT Pus Ukumbini


Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akitoa mwongozo wa kuanza kwa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma.


Taswira ukumbini
  • Picha tumeshirikishwa na Binagi Media