Dk Mwakyembe alisema hayo jana kwenye mahojiano katika kipindi cha 360 kinachorushwa moja kwa moja, asubuhi siku za wiki na Televisheni ya Clouds.
“Tuna kesi 176 za kuhujumu uchumi tangu Juni mwaka jana hadi sasa. Kesi 13 zimekamilika, watu 12 wamehukumiwa vifungo vya jela na tunawadai Sh29 bilioni kwa hiyo kama mtu alikuwa na ‘kastore’ tutauza tupate hiyo pesa,” “Nchi ilipofikia tunataka tuachane na hizi tabia za udokozi unapopewa mamlaka ya kuhudumia umma.”Alipoulizwa kuhusu mahakama ya mafisadi alisema:
“Hatujaanzisha Mahakama, tumeanzisha divisheni (kitengo) ambacho kitasimamia kesi hizo kwa haraka na kwa weledi zaidi.”