Madawati hafifu yakataliwa; RC awa mbogo; Mbunge asema watakataa na miradi yote iliyo chini ya kiwango


Madawati yaliyotengenezwa kwa ajili ya shule zilizoko Kilolo mkoani Iringa, yamekataliwa kwa kutengenezwa bila kukidhi viwango.
"Haya madawati yenu siyataki. Siyataki kabisa. Hatukuwa tunatengeneza madawari ya mchezo kuigiza." 
"Hayo madawati yasisambazwe mashuleni, na waliyoyasambaza waende wakayachukue wayarejeshe hapo kwenye karakana. Hivi mpaka wanatengeneza madawati yanafika 600+ hapakuwepo Mtendaji wa Kata? Hakuwepo Katibu Tarafa? Hapakuwepo na Mkuu wa Wilaya? Hapakuwepo na Mkurugenzi? Hapakuwepo na Diwani aliyepita kuangalia madawati? Lakini je, hapakuwepo na Afisa Elimu ambaye ndiye mwenye idara yenyewe? Hili ni jambo kubwa. Kama kwenu mnaliona dogo, lakini mimi kwangu ni jambo kubwa. Kinachofuata ni jambo ambalo litamshangaza kila mmoja wenu. Hamuwezi ninyi kunifanya niandike kwenye taarifa kuna madawati yapo kwenye karakana yanatengenezwa, kumbe madawati yanayotengenezwa kwenye karakana hayakidhi kiwango cha madawati tunayohitaji. Lakini kumbukeni, mmetumia kulipa fedha za serikali. Mtazirejesha! Wala kwenye hili hatubembelezani. Mtazirejesha." alisema Mkuu wa Mkoa, bi. Amina Masenza.