Mkuu wa Mkoa atembelea patakapochimbwa madini adimu ya vifaa vya ndege na kompyuta

RC Amos Makalla akitembezwa na Mkurugenzi wa Panda Hill Limited, Derick katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya. (Picha E. Madafa; D.Nyembe)
Na Mwandishi wetu, Mbeya 

Mkuu wa mkoa wa Mbeya bwana Amos Makalla ametembelea eneo la Panda Hill lililoko katika Kata ya Songwe mkoani Mbeya, mahali ambapo patachimbwa madini adimu aina ya niobium ambayo hutumika kutengeneza vifaa vya ndege na kompyuta.

Mpaka sasa madini hayo huchimbwa kwenye bara la Amerika tu, hivyo kugundulika kwa madini hayo Tanzania kunaifanya nchi hii kuwa mgodi wa nne duniani na wa kwanza barani Afrika

Mkurugenzi wa kampuni ya Panda Hill Limited ndugu Derick amesema imewachukua zaidi ya miaka mitan5 kufanya utafiti na kugundua uwepo wa madini hayo. Amesema taratibu zote za kisheria zimekamilika na kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika mradi huo. Pia amesema kuwa mradi huo utatengeneza ajira kwa watu 500 wakati utakapoanza uzalishaji mapema mwaka 2018.

Mkuu wa mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ugunduzi na uwekezaji huo mkubwa sanjari na kuwataka na kutoa ushirikiano na ushirikishwaji wa kwa viongozi na wananchi kwa kila hatua ili kuweka wazi mradi huo kwa wananchi.

Aidha, amewataka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ili wananchi wanaozunguka eneo hilo, uzalishaji utakapoanza, wafaidike na ajira, huduma za jamii na kodi mbalimbali kwa halmashauri na serikali kuu.

Pia amewashukuru kwa mchango wa madawati 400 ambayo yatasambazwa kwa shule 7 zilizokuwa na upungufu wa madawati

Kwa mujibu wa taarifa za wataalam, madini ya niobium huchanganywa na metali nyingine na vyuma vyake kutumika kwenye ujenzi bomba la kupitishia mafuta na metali zake kutumika katika injini za ndege ili kuzuia mitambo yake kupata joto kali.

Gereza kuhamishwa kupisha mgodi  Imeandikwa na ELIUD NGONDO, MBEYA via MTANZANIA

GEREZA la Kilimo la Songwe lililoko mjini Mbeya, litahamishwa ili kupisha uchimbaji wa madini ya niobium yaliyopo eneo hilo.

Taarifa hiyo ilitolewa mjini hapa jana na mwakilishi wa Kampuni ya Panda Hill, inayotarajia kuchimba madini hayo, Emmanuel Kisasi.

Kisasi alisema kwamba watahamisha pia nyumba za wafanyakazi wa gereza hilo.
“Kwa kuwa eneo lilipo gereza hilo kuna madini, kampuni yetu ya Panda Hill imetenga shilingi bilioni 400 kwa ajili ya kuhamisha gereza hilo, ikiwa ni pamoja na nyumba za watumishi kwa umbali wa kilomita tano.
“Sambamba na hilo, zaidi ya wananchi 467 waliopo maeneo ya mgodi, wanatarajia kunufaika kwa kupata ajira mara tu uchimbaji utakapoanza mwaka 2017.
“Madini hayo tunayotarajia kuyachimba yatatumika kutengeneza vitu vya chuma, kulainisha vyuma na kuwa imara zaidi na pia yanatumika kwenye ujenzi wa nyumba.
“Pia, yatatumika kutengeneza vifaa vya ndege, mabomba ya mafuta, mabomba ya gesi, lensi za kamera pamoja na vifaa vya kompyuta.
“Kwa hiyo, utafiti tulioufanya tumegundua kuna tani milioni 96.3 za madini hayo na yatachimbwa kwa zaidi ya miaka 30,” alisema Kisasi.
Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza, alisema kuwapo kwa mgodi huo, kutawasaidia wananchi wa jimbo lake kubadilika kuchumi.


Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla aneo ambalo litachimbwa madini hayo.

Ramani ya mradi

Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ramani itakayotumika katika mradi huo

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza jambo na viongozi wa kisiasa, kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya mbeya, uongozi wa kampuni ya Pandahil limited ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya

Mwakilishi wa kampuni ya Pandahil limited Mbeya Emanuel Kisasi ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la mradi eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya

Eneo ambalo litahusika kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Mwisho.