Mkuu wa Wilaya asimamia zoezi la kubomoa nyumba zilizo karibu na mgodi wa Acacia

Mkuu wa Wilaya akielekea eneo lenye nyumba hizo
Mkuu wa wilaya ya Tarime, GLORIOUS LUOGA, ameendesha zoezi la ubomoaji nyumba zaidi ya 300 zilizokuwa zikikaliwa na wakazi wa kijiji cha Nyabichune kilichopo nyamongo wilayani tarime mkoani mara baada ya mgodi Acacia North Mara kukubali kuwalipa wananchi wa kijiji hicho kiasi cha shilingi billioni nne na milioni mia saba ikiwa ni fidia ya kuwaondoa wananchi hao wanaozunguka eneo hilo la mgodi.

Picha zote: Shommi B blog


Sehemu ya nyumba zilizovunjwa

Nyingine zilikuwa karibu kabisa na eneo la machimbo

Maagizo ya uvunjanji yanatolewa

Meneja uendelezaji idara ya ardhi wa mgodi wa Acacia North Mara,Abel Yiga, akimuonesha orodha ya majina ya wananchi walioandaliwa malipo na kuiomba serikali kusaidia kuona wananchi hao hawatumii fedha hizo kwenda kujenga nyumba nyingine maeneo ya mgodi maarufu kwa jina la "tegesha"ili kuepuka migogoro.

Majina yakisomwa

Wananchi wakisikiliza majina ya walipwaji


Kazi inaendelea


Kazi inaendelea