Orodha ya majina ya Magazeti 473 yaliyofutiwa usajili na Serikali

Waziri Nnauye akionesha kwa waandishi wa habari tangazo la serikali Na. 65 linaloonesha kusudio la kufuta viapo vya usajili wa magazeti ambayo hayajachapishwa kwa muda wa miaka mitatu kwa mujibu wa sheria ya magazeti leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi. Flora Mwenyembegu. (Picha na: Genofeva Matemu)
Na: Frank Mvungi

Serikali imefuta usajili wa magazeti 473 kupitia tangazo lake lililochapishwa katika Gazeti la Serikali lenye namba 195, (Supplement No. 23) la tarehe 10/06/2016 kutokana na Magazeti hayo kutochapishwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam.

Mhe. Nnauye alifafanua kuwa kutokana na kufutwa kwa viapo vya usajili wa magazeti hayo, mtu yeyote atakayechapisha au kusambaza magazeti yaliyotajwa katika tangazo hilo kwa njia ya nakala ngumu au kieletroniki atakuwa anakiuka sheria ya magazeti sura ya 229 kifungu cha 6 na hivyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Iwapo kuna mmiliki wa gazeti ambaye angependa kuendelea na biashara hii baada ya kufutwa magazeti hayo, milango iko wazi kwa ajili ya kuwasilisha maombi mapya ya usajili kwa kufuata taratibu zilizopo” alisisitiza Mhe. Nnauye.

Akifafanua Mhe. Nnauye amesema kuwa wamiliki wa magazeti 473 yakiwemo Alasiri, Pambamoto, Mipasho, Mirindimo, na Taifa Tanzania ambao viapo vyao vimefutwa, wahakikishe kwamba hawavunji sheria kwa kuanza biashara hii ya magazeti bila kufuata taratibu za kujisajili upya na endapo watakiuka maelekezo hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa mujibu wa kifungu cha 23 (1), Waziri mwenye dhamana ya kusimamia sekta ya Habari amepewa mamlaka ya kufuta hati za viapo zilizoandikishwa na gazeti ambalo halikutolewa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo baada ya kutangaza kusudio la kuyafuta magazeti husika kupitia Gazeti la Serikali.

Wizara imefanya mapitio ya viapo vya usajili wa magazeti yote na Ofisi ya Waziri mwenye dhamana ya Habari imejiridhisha kuwa kuna idadi ya magazeti 473 ambayo yamesajiliwa lakini hayajachapishwa kwa zaidi ya miaka mitatu.

Kufuatia hali hiyo, tangazo la serikali Na. 65 la tarehe 22 Machi, 2013 lilitolewa kwa ajili ya kutangaza kusudio la kufuta viapo vya usajili wa magazeti 550 na kupewa fursa ya kujitetea au kuonyesha nia ya kuendelea kuchapisha.

Baada ya tangazo hilo magazeti 77 yalionyesha nia yakuendelea kuchapisha, kwa mantiki hiyo hadi sasa kufuatia orodha ya wakati huo pamoja na kupewa muda mrefu zaidi ya unaotakiwa kuna magazeti 473 ambayo hayachapishwi na yamekosa sifa ya kuendelea kutambulika na msajili wa magazeti kwa mujibu wa sheria.

Aidha Mhe. Nnauye ametoa pongezi kwa wamiliki wa vyombo vya habari ambao wamekuwa wakifuata sheria na taratibu zinazosimamia tasnia ya habari ili kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi kwani Serikali inathamini sana mchango wa huduma ya vyombo hivyo.

Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya Msajili wa Magazeti iliyopo chini ya Idara ya Habari (MAELEZO), Tanzania inayo magazeti na majarida 881 yaliyosajiliwa kisheria. Hata hivyo licha ya magazeti na majarida kusajiliwa yapo baadhi yameshidwa kuchapishwa na wamiliki mara baada ya kusajiliwa na mengine yalichapishwa kwa muda mfupi na kuacha kabisa uchapishaji.

Orodha ya majina ya Magazeti 473 yaliyofutiwa usajili na Serikali baada ya kutochapishwa kwa muda wa miaka mitatu.

Orodha ya magazeti hayo ni:

1. Sports Scene
2. Uzazi Bora
3. Elimu Haina Mwisho
4. Habari Maalum ya Uzima Tele
5. Lengo
6. Lishe
7. Mfanyakazi Huru
8. Mapinduzi ya Kijamaa
9. Ngao
10. Uhuru na Amani
11. International Diplomacy
12. Pambamoto
13. Tanztravel
14. Carmel
15. Sky Safety
16. Sauti ya Amani
17. Professional Accountant
18. AAT Newsletter
19. Elimu ya Afya
20. Family Mirror
21. Sauti ya Siti
22. Materials Management Journal
23. Contact Magazine
24. Miombo Newsletter
25. Mkulima
26. Weekend Magazine
27. ALAT Magazine
28. Uhai wa Mtoto
29. Kilimo Leo
30. Kahawa News
31. Usangu Leo
32. Drug Information Bulletin
33. Michapo
34. TCMA Newsletter
35. Track News
36. Gazeti la HESAWA
37. Aids link Newsletter
38. Maranatha
39. Sauti ya Maendeleo
40. Students Voice
41. Ham
42. Mama na Mtoto Kigoma
43. Ita Jamii
44. Shaba
45. Maendeleo ya Jamii
46. Kilimanjaro Leo
47. Rasilimali
48. Ija Webonere
49. Habari za Kibaha
50. Trade and Industry in East and Central Africa
51. Pan-Africa Lutheran Information
52. Pamba Yetu
53. Announcer
54. Juhudi
55. Meida Habari
56. Tujifunze
57. Tujiendeleze
58. Tujielimishe
59. Elimu Yetu
60. Nyegezi Weekly News
61. Jenga
62. Mjumbe wa UNESCO
63. Wasaa
64. Nguvu Kazi
65. Tanzania Dental Association Newspaper
66. Journal of Building and Land Development
67. Hiari
68. Federation Samachar
69. Tanzania Engineers
70. Journal of Cooperative and Business Studies
71. Twiga News
72. Pambazuko
73. Tanzania Bankers Journal
74. I.E.T. Newsletter
75. Tanzania Medical Journal
76. Elimu ni Bahari
77. Watu
78. Ushindi WETU
79. N C.S.W.S Newsletter
80. HEKO
81. T.W.C.A Newsletter
82. Sunday Times
83. Chombeza
84. Amua
85. Uhai
86. Africa Link
87. Uamsho
88. Ushirika Wetu
89. Wiki hii
90. Rockers
91. Renewable Energy & Environment News
92. Financial Times
93. Mzizima
94. Tabasamu
95. Pasua
96. Uhifadhi-Kanda ya Serengeti
97. Femina Magazine
98. Programu ya Elimu ya Uraia
99. Sauti ya Demokrasia
100. Evening News
101. Mbiu ya Kolping
102. Leo
103. Jua
104. Mageuzi
105. NETF Newsletter
106. Alasiri
107. I IT Newsletter
108. Sauti ya Kisanji
109. Raia
110. Dar Leo
111. Mchunguzi
112. Alfajiri
113. Baragumu Tanzania
114. Mbiu ya Uchaguzi
115. Mwangaza
116. Great Lakes Analysis
117. Tuzungumze
118. Ujumbe wa Moyo Mtakatifu wa Yesu
119. Straight Talk/Sema Waziwazi
120. Msafara
121. Health Education Forum
122. Funster
123. Ulingo wa jinsia
124. Wajenzi Newsletter
125. Mapambazuko
126. Matukio Daima
127. Bayana
128. Faith Magazine
129. Yesu ni Jibu
130. Amani
131. Jambo
132. Tamasha
133. Ambha
134. Cheko
135. Bahari
136. Agenda
137. Change
138. Kumekucha Kilimanjaro
139. Al-Jumua’h
140. Haki
141. Lumen
142. Shinyanga
143. Daraja
144. The Star
145. Biashara Mbeya
146. Fukuto
147. Leo ni leo
148. Wakati
149. Kajumulo Michezo
150. The Contractor
151. Mererani Leo
152. Mirindimo
153. Privatisation
154. Mkristu
155. Cane and Sugar Journal
156. Advertise Weekly
157. Shauku
158. Malezi
159. The Road User Magazine
160. Harakati za Walemevu
161. Mfugaji wa Kagera
162. The People
163. Jitambue
164. Leonardo Da Vinci
165. Capital
166. Hamu
167. Kamtu
168. What’s Happening in Dar Es Salaam
169. The Accountant Journal
170. Buy and Sell TZ
171. ED-SDP Newsletter
172. Tega Sikio
173. Mwambao
174. Ari Mpya
175. IN & ON
176. Utamu
177. TAA
178. Kwetu
179. Tausi
180. CSSC News
181. Njia
182. Kidedea
183. Afrika Mashariki
184. Burudisho la Wiki
185. The Crane
186. Harambee
187. Radi Tanzania
188. IT Vision
189. Mipasho
190. Quarterly Update
191. Tumaini Hill
192. Bakora
193. Muelimishaji
194. African Travel Review
195. Mchumi
196. Tanzania Guide
197. Ajira
198. Mwanza Environment/Mazingira
199. Tangaza Leo
200. Mbeya Leo
201. Sauti ya Wakulima(KCU(1990)Ltd.
202. Mama Afrika
203. Mwadeta
204. Ehabi
205. Dhamira
206. The Tanzania Journalist Newsletter
207. The Insurer
208. Tanzania Science & Technology News
209. Tanzania Leo
210. Business Promoter
211. Ushindi wa Ajabu
212. Shabaha
213. TTCL Review Solutions for Practical Managers
214. Kauli
215. Tanzania Trade Directory
216. The Image
217. Faraja
218. Tochi
219. Tan T2 Newsletter
220. Mhakiki
221. Taswira
222. Sakata
223. Zungu
224. Tanzania Business & Tourist Guide
225. Tanzania Business Review
226. Shani
227. Maadili
228. Mchana
229. Mema
230. Tamtam
231. Star Sport Tanzania
232. Elimu
233. Reaching Tanzania
234. Jitegemee
235. Daily Times Tanzania
236. Mission Echo
237. Sauti ya Dodoma
238. Dala Dala
239. PR Magazine
240. Hallo
241. Advertising Tanzania
242. MISA Focus
243. Maswa Leo
244. Uzima
245. Nitangaze
246. Jicho Letu
247. Mwanamke
248. Sikiliza
249. Mwanasimba
250. Taswira ya Maisha
251. Ulimwengu
252. Jumatatu
253. Chaguo
254. The Great Lakes of East Africa Business News
255. Shirikiana
256. Mazingira Moshi
257. Advertising Africa
258. Mfuko News/Habari za Mfuko
259. Jamii Yetu
260. Consumer Digest
261. Cheza
262. Karatu Leo
263. Nyota ya Spoti Tanzania
264. Sayari Mpya
265. C.E.D Newsletter
266. Kiki East Africa
267. Habari Njema
268. Angalizo
269. Living
270. Events & Leisure
271. Sani Spoti
272. Mkereketwa
273. Leat News
274. Msomi
275. Bembea Tanzania
276. Pwani Wiki Hii
277. Hali Halisi
278. Zeze
279. Moto Moto
280. Mkweli
281. Fleva
282. Jungu Kuu
283. Kanisa Letu
284. Tunzarika
285. The Educator
286. Mwanza Where About
287. Biz ‘N’ Leisure
288. Yuppies Weekly
289. Kabumbu
290. Ua Jekundu
291. Focus On
292. Life
293. Entaprena
294. Banking and Finance
295. Mkombozi
296. Tanzania Yetu
297. Mwanafunzi
298. The Architect and the Quantity Surveyor
299. UDSM Gender Program Newsletter
300. Deiwaka
301. Discourse on Science Religion & Development
302. Tujenge Tanzania
303. Kilimanjaro Post
304. Kilimanjaro Yetu
305. Kitu Halisi
306. Mtazamo
307. Sayari
308. Education in Focus
309. Admedia Magazine
310. The Mediator
311. Reflections
312. Wekeza Sasa
313. Sun Energy
314. Visa
315. Chaneli ya Michezo
316. Bonanza
317. Youth Leadership Training Program, YLTP Newsletter
318. Nyumbani
319. Bure
320. Horizon
321. Trader
322. Mesenja
323. Jobs & Tenders
324. Fly Safe
325. Za Leo
326. Lulu
327. Nahodha
328. Elimika
329. Samba
330. Arusha Raha
331. Dakika 90
332. Tikisiko
333. The Bongo Sun
334. Mwana Afrika
335. Acha Umbea
336. Kiwanda
337. Farmers Media
338. Tulonge
339. Utatu
340. Nyundo ya Jamii
341. Excel Magazine
342. What On
343. BSS Magazine
344. Kigoma Yetu
345. The Entertainer
346. Arusha 2 Day
347. Jahazi
348. Homes and Property Tanzania
349. Money and Banking
350. Ndoto
351. Morning News
352. Jibu la Maisha
353. Young Spoti
354. The Simplifier
355. Pata Ukweli
356. The Executive
357. Taifa Tanzania
358. Drugs and Health
359. Delivery
360. Health and Fitness
361. Msonge
362. Mechi
363. Engineering News
364. Voice of Haki
365. The Base
366. Urembo Shop
367. Asubuhi Njema
368. Namba 10
369. Mjumbe Hauwawi
370. Property and More Advertisement
371. The Business Partner
372. Goli la Ndoto
373. La Dezo
374. Dunduliza
375. Tanedu ORG
376. Timiza
377. Tanga Yetu
378. Tanzania Advertiser
379. Tan Properties
380. Reality Magazine
381. The Tanzanian Lawyer
382. Mtandawazi
383. Mvuja Jasho
384. Mashua
385. Saa
386. Familia
387. What Car?
388. Mwongozo
389. Tathmin
390. Property Guide
391. Sauti ya Uwamadar
392. Miwani
393. Msafiri
394. Chimbuko
395. Medani ya Michezo
396. Gumzo
397. Tanzania Health Magazine
398. Rafiki Yako
399. Wakili Bulletin
400. Mwanasoka
401. Mwamini Mungu
402. The Corporate Tanzania
403. SMEs Focus
404. Mwanangu
405. Muungwana
406. Schools and Colleges
407. Health Focus
408. Safari Leo
409. Sauti ya Wazee
410. Sura ya Mtanzania
411. Mwanajamii
412. Ufunuo
413. Upako
414. City Advert
415. Haki Bulletin
416. African Communication Research
417. Tanzania Organic Today Newsletter
418. Tanzania Automobile Magazine
419. Jifunze
420. Darubini ya Uchaguzi
421. Election Monitor
422. Auto Trader Tanzania
423. Karibu
424. Education Review
425. Mfuko wa Elimu
426. Mwamko
427. Mkakati
428. The Seasonal Advertiser
429. Weekly Deals
430. Zika Ukimwi Usikuzike
431. Mwadilifu
432. Tanzania Procurement Times
433. Spoti Duniani
434. True Life Magazine
435. Msuluhishi
436. Whats’s Tanzania
437. Acha
438. Haiba
439. TAA ya TAN-HOPE
440. Tanzcom
441. Tokomeza
442. Kilimo Endelevu
443. Mamboleo
444. Chekenao
445. Duniani Leo
446. Sauti ya TUICO
447. Mazingira Arusha
448. Spotistaa Afrika ya Mashariki
449. Jikomboe
450. Mshauri Wako
451. Taphgo Newsletter
452. Dar Search Magazine
453. Mtafutaji
454. Sauti ya Jimbo kuu la Mwanza/Mwanza Calling
455. Kaya
456. Bantu Comics
457. Yanga Imara
458. Environews Tanzania
459. Harakati Mitaani
460. Zinduka
461. Habari za Tanzania
462. Macho
463. Jamii Express
464. Falsafa
465. Academia
466. The Investor
467. Starehe
468. Raha
469. TCCIA Newsletter
470. The East African Times
471. Vision Tanzania
472. Fiesta
473. Buy Me