Sabuni zitokanazo na mchikichi KigomaSabuni mara nyingi tumezoea kuziona zikitengenezwa na viwanda vikubwa nchini na kupakiwa katika maboksi nadhifu. Lakini kumbe kila mtu anaweza kuwa na kiwanda kidogo cha kuzalisha sabuni nyumbani kwake na kuwauzia majirani zake na kujipatia kipato yeye na familia yake baada ya kupata ujuzi maalum kutoka kwa watalaam.

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ni mingoni mwa mashirika na taasisi ambazo zimekuwa zikiwafundisha wananchi mbalimbali kuendesha viwanda vidogo vidogo na kufanya kazi za mikono pamoja na usindikaji kutokana na malighafi ambazo zinapatikana katika maeneo yao.

Akina mama wa Kigoma ni mingoni mwa waliopata ujuzi huo na sasa wao wanazalisha sabuni zitkanazo nazo mabaki ya michikichi baada ya kukamuliwa mafuta. Bei ya mche mmoja wa sabuni hii ni Sh 1,000. 

Uzalishaji wa sabuni hizo umeongeza pato la wakuliwa wa michikichi ambao awali walikuwa wakitegemea zaidi mapato kutokana na mafuta yake.


Katika baadhi ya mitaa mjini Kigoma ukipita huwezi kukosa aina hii ya sabuni ikiuzwa kwa wingi. Wauzaji wake ni akina mama na watoto ambao husaidia wazazi hao kufanya bishara hiyo na kukuza pato la familia, licha ya changamoto za soko la uhakika.Mbali na mkoani Kigoma, sabuni hizi hivi sasa zinapatikana katika maeneo mengi nchini. 

Sabuni hizi zina majina mawili ya MZAZI na BORA. Hayo ni majina ya mihuri tu lakini si kuwa zinazalishwa na watu wawili bali kila mtu huzalisha kivyake na kupiga mihuri hiyo.