Serikali kuandika kitabu kumhusu John Stephen Akhwari aliyesema, 'My country did not send me 5000 miles to start the race; they sent me 5000 miles to finish the race"

John Stephen Akhwari aliyeiwakilisha Tanzania kwenye Olimpiki iliyofanyika Mexico mwaka 1968
Serikali ya ahidi kuandika kitabu cha historia ya michezo Mwanariadha mzalendo John Stephen Akhwari kutokana na mchango wake mkubwa wa kupeperusha vyema bendera ya nchi.

Ahadi hiyo imetolewa leo Wilayani Babati na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura alipokuwa katika ziara ya kikazi iliyolenga kukutana na wadau wa kisekta na kushauriana namna ya kuboresha sekta zilizopo chini ya wizara.
“Mzee John Stephen Akhwari anakila sababu ya kutengezewa kumbumkumbu ya kitaifa itakayo tumika kufundisha suala la uzalendo kwa wanamichezo pale wanapokuwa katika mashindano mbalimbali iwe ndani ya nchi au nje kwani kauli kwa kauli yake ya “Sikutumwa na nchi yangu mbio bali nimetumwa kumaliza mbio” kauli hii ni kielelezo kikubwa cha uzalendo aliyokuwa nao,”alisema Naibu Waziri Wambura.
Pamoja na hayo Naibu Waziri alisema Mwanariadha huyo zamani amefanya mambo mengi makubwa katika historia ya riadha dunia ikiwa ni pamoja na kufungua mashindano ya Olimpiki nchini Beijing katika mwaka 2008 kwa kuzungusha Mwenge wa Olimpiki Uwanjani,na hili ni jambo kubwa la kujivunia kama nchi.

Halikadhalika Naibu Waziri alisisitiza kwa kusema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha inahifadhi rekodi za wanariadha wote waliyoletea nchi sifa katika mashindano ya Kimataifa na lengo ni kufanya sekta hii ya riadha inakuwa rasmi nakufahamu rekodi zake.
Mitandaoni amenukuliwa na kuandikwa katika tovuti kadha wa kadha. Huu ni usemi wake uliopata umaarufu duniani kote...