Taarifa ya habari ChannelTEN Julai 12, 2016

Jana niliandika masikitiko yangu kwa kutokuweza kutizama video hizi za taarifa ya habari, baadaye niliwaza mbinu nyingine rahisi baada ya kujaribu kutumia huduma za "anonymous IP address" na kukwama, niliweka VPN kwenye simu yangu (simu yangu inatumia Android OS na VPN apps zipo Google Play), nikai-turn on, kisha nikaenda kwenye taarifa za habari, na nilifanikiwa kuzisikiliza zote. Ikiwa una tatizo kama hilo na unataka kutizama video hizi, fanya nilivyofanya.