Tanzania hands over potential wreckage from missing plane to Malaysia
Tanzania's Civil Aviation Authority on Friday handed over to Malaysian officials a piece of debris potentially from a Malaysia Airlines plane that went missing in 2014.

Flight MH370, which had 239 people on board, had been en route from Kuala Lumpur to Beijing.

Malaysian officials had travelled to Dar es Salaam to collect the piece of a wing found off the Tanzanian island of Pemba. Its discovery was announced in June, with Malaysian officials saying it was the biggest fragment linked to the missing aircraft so far.

Malaysian Transport Ministry investigator Aslam Basha Khan said in Dar es Salaam that it was too early to say whether the fragment came from the lost aircraft.

He said Malaysia was currently investigating wreckage found in Mozambique, Madagascar, Mauritius and South Africa.

John Feakes, the Australian high commissioner to East Africa, said Australia was leading the investigation into the missing plane.

Pieces of the plane found on coastlines around the Indian Ocean indicate that it may have crashed south-west of Australia. [aboutcroatia.net]

SERIKALI YA TANZANIA YAKABIDHI MABAKI YA BAWALA LA NDEGE LILILOKOTWA PEMBA MWEZI JUNI 2016 KWA SERIKALI YA AUSTRALIA NA MALAYSIA KWA USHUNGUZI RASMI. BAWA HILO LINADHANIWA KUWA LA NDEGE YA ABIRI YA MALAYSIA MH370 ILIYOPOTEA MACHI 2014Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho, (katikati) akizungumza na waandishi wa habari, wakati Tanzania ilipokuwa ikikabidhi bawa la ndege kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba Chungua Hamad Chungua (hayupo pochani) mwezi Juni 2016. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi mwandamizi wa ajali za ndege , Wizara ya Uchukuzi Malayasia, Aslam Basha Khan, Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John Feakes na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari. Hafla hiyo ilifanyika Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho (katikati) akizungumza na waandishi wa habari, wakati Tanzania ilipokuwa ikikabidhi bawa la ndege kwa serikali ya Malaysia. Kutoka kushoto ni Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John Feakes na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari.

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho (katikati) akimsikiliza kwa makini Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John Feakes (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari, akiishukuru serikali ya Tanzania wakati ilipokuwa ikikabidhi bawa la ndege kwa serikali ya Malaysia Kutoka kushoto ni Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John Feakes na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari.

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,(wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari ,pamoja na Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John Feakes (wapili kushoto) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi mwandamizi wa ajali za ndege wa Wizara ya Uchukuzi Malayasia, Aslam Basha Khan, wakati akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) wakati serikali ya Tanzania ilipokuwa ikikabidhi bawa la ndege kwa serikali ya Malaysia

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,(kulia) akishuhudia Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akisaini hati ya makabidhiano ya mabaki ya bawa la ndege wakati serikali ya Tanzania ilipokuwa ikikabidhi bawa hilo kwa serikali ya Malaysia. Kulia ni Mwanasheria wa Mamlaka na Katibu wa Bodi ya wakurugenzi wa TCAA,Vallery Chamulungu.

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,( wapil kulia) na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari (kulia) wakifuatilia kwa mdhamini wakati Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John Feakes (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano. Aliyesimama ni Mwanasheria wa Mamlaka na Katibu wa Bodi ya wakurugenzi wa TCAA,Vallery Chamulungu.

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho, (wanne kulia) Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari (watano kulia) Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John Feakes (watatu kushoto), Mkurugenzi mwandamizi wa ajali za ndege, Wizara ya Uchukuzi Malayasia, Aslam Basha Khan, (wapili kushoto), Mwanasheria wa Mamlaka na Katibu wa Bodi yawakurugenzi wa TCAA, Vallery Chamulungu (kushoto) pamoja na maafisa wa kitengo cha ukaguzi wa ajari za ndege Wizara ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano wakikabidhiana.

Mkurugenzi mwandamizi wa ajali za ndege , Wizara ya Uchukuzi Malayasia, Basha Khan, (kushoto waliochuchuma ) na Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,wakikagua mabaki ya bawa la ndege, wakati serikali ya Tanzania ilipokuwa ikikabidhi bawa hilo kwa serikali ya Malaysia. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari na Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John Feakes.

Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari (kulia ) akisaidiana na wafanyakazi wa DHL kuingiza mabaki ya bawa la ndege tayari kuelekea nchini Malaysia kwa uchunguzi zaidi mara baada ya serikali ya Tanzania kulikabidhi bawa hilo kwa serikali ya Malaysia

Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari (wapili kushoto ) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa DHL jinsi ya kuingiza mabaki ya bawa la ndege tayari kuelekea nchini Malaysia kwa uchunguzi zaidi mara baada ya serikali ya Tanzania kulikabidhi bawa hilo.