David Mgwasa (kushoto) na Deogratius Lazari |
SHIRIKA la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART), imetangaza kuwa terehe Julai 30 mwaka huu ndiyo mwisho wa matumizi ya tiketi za kawaida kwa abiria, na badala yake zitatumika kadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwasa ametoa taarifa hiyo alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, asubuhi ya Jumapili ya Julai 10, 2016.
"Tiketi zitaendelea kutumiwa na wanafunzi lakini watu wengine wote watatumia kadi maalumu za kupandia mabasi yetu" alisema Mgwasa.Alisema UDART imepunguza bei ya kadi hizo kutoka sh. 4,500/= ya awali hadi kufikia sh. 2,000/= ili kutoa fursa kwa kila mwananchi kuweza kuipata kadi hiyo na kuitumia.
Mgwassa alisema kadi zilizouzwa ni 55,000 na zilizobaki ni 150,000.
Mkuu wa idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo iliyoingia ubia ma UDART katika mpango huo, Deogratius Lazari alisema wateja wataweza kulipia kadi hizo kupitia kwa mawakala wao waliopo katika vituo vyote vya UDART na kwa njia ya mitandao yote ya simu.