Waziri Tizeba asimamisha kazi watendaji 6 Wizara ya Kilimo na kumvua 1 madaraka, kumhamisha


Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba amemsimasha kazi Mtendaji Mkuu wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula Bw. Charles Walwa na watendaji wengine watano ili kupisha uchunguzi kufuatia kuwepo kwa tuhuma za kuhujumu Hifadhi ya Taifa ya chakula.