Ziara ya Balozi Masilingi katika jimbo la Washington

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa kwenye mkutano na Watanzania Seattle jimbo la Washington nchini Marekani siku ya Jumamosi July 16, 2016. Habari na Picha na Katunda Catunda Mwakilishi wa Vijimambo Seattle, WA
Na Katunda Catunda

Balozi wa Tanzania nchi ni Marekani muheshimiwa Wilson Masilingi yupo ziarani katika jimbo la Washington alipata fursa ya kuzungumza na jumuiya ya watanzania waishio hapo ambapo alieleza mikakati ya ziara hiyo ni kupanua Milango ya kibiashara Kati ya Tanzania na Marekani kutokana na kuwa jimbo la Washington ni moja ya majimbo ambayo ni makao makuu ya makampuni makubwa duniani

Katika Ziara hiyo alitembelea kiwanda cha ndege cha Boeing na kupanga mikakati ambayo serikali ya awamu ya tano inatarajia kununua ndege mbili za kisasa ili kufufua shirika la air Tanzania ,pia alipata nafasi ya kutembelea Microsoft na kampuni ya Starbucks ambayo inaendesha migahawa mikubwa ya kahawa duniani. Balozi Huyo alimaliza mazungumzo yake kwa kukutana na Chama cha wafanyabiashara cha Seattle .

Ziara hizo ni moja mikakati ya serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli katika kupunguza matumizi ya serikali kusafirisha viongozi kutoka Tanzania kuja kufanya mazungumzo badala ya kutumia Mabalozi na wawakilishi waliopo kwenye nchi hizo


katibu wa jumuiya ya watanzania Seattle (Tanzaseattle) Hajji Rajab Hajji akimkaribisha balozi

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiongea kwenye mkutano na Watanzania Seattle jimbo la Washington nchini Marekani siku ya Jumamosi July 16, 2016.

Wakati wa chakula.

Watanzania Seattle wakifuatilia mkutano na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi siku ya Jumamosi ya Julai 16, 2016.

Mkutano ukiendelea.

Watanzania Seattle wakimsikiliza katibu wa Jumuiya ya Watanzania Hajji Rajab Hajji alipokua akimkaribisha Mhe. Balozi.

Mkutano ukiendelea