Afisa polisi wa Marekani akamatwa kwa kundi la ISIS

Idara ya sheria ya marekani siku ya Jumatano ilitangaza kukamatwa kwa polisi mmoja wa mji mkuu wa Washington DC kwa shutuma za kujaribu kutoa msaada kwa kundi la Islamic State imeripoti Sauti ya America.

Afisa huyo mwenye umri wa miaka 36 kwa jina la Nicholas Young na anayefanya kazi kwenye kitengo cha usafiri wa mji maarufu Metro, anashukiwa kumpatia afisa wa jinai aliyejificha, kadi za zawadi zenye dhamani ya dola 250 na ambazo zilikuwa na maandishi ya siri yanayotumiwa na kundi la ISIS kutoa mafunzo kwa wanachama wapya.

Hati ya kiapo inasema Young, aliyenza kufanya kazi ya polisi mwaka wa 2003, aliwahi kuzurua Libya mara moja mnamo mwaka wa 2011, na alikuwa akijaribu kutembea tena kwa mara ya pili. Amekuwa aifuatiliwa kwa karibu na idara ya upelelezi ya FBI tangu mwaka wa 2010.