Agizo la Mkuu wa Mkoa Mbeya kuhusu mikutano ya kisiasa

Mikutano ya Operesheni UKUTA iliyotangazwa kuratibiwa na Chadema kuanzia Septemba Mosi, imepigwa marufuku na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla -- gazeti la MWANANCHI limeripoti.

Akizungumza katika kikao cha kazi kilichoshirikisha kamati ya ulinzi na usalama mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri, Makalla ametangaza kupiga marufuku mkutano wowote utakaofanyika chini ya utaratibu unaoitwa Operesheni UKUTA.
“Bila shaka wananchi Mbeya wanataka amani na kazi, hivyo ni marufuku kufanyika mkutano wowote wa kisiasa unaoandaliwa kwa kushirikiana na watu wengine kutoka nje ya mkoa,” amesema Makalla aliyewahi kuwa mbunge na mweka hazina wa CCM.