Askari FFU aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa kumuua Mwangosi akata rufaa

Pacificius Simon (kulia)
ASKARI wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon (27) aliyefungwa miaka 15 kwa kuhusika na mauwaji ya bila kukusudia dhidi ya mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten Daudi Mwangosi amekata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama kuu kanda ya Iringa chini ya jaji Dk Paulo Kiwelo mtandao wa matukiodaimaBlog umeelezwa.

Rufaa hiyo imekatwa siku mbili toka ilipotolewa hukumu hiyo na wakili wake wa utetezi , Lwezaula Kaijage ambaye siku ilipotolewa hukumu hiyo alisema ni mapema mno kuzungumzia hatua atakayochukua baada ya hukumu hiyo.
“Kesi siyo ya kwangu ni ya mshtakiwa, mimi nilikuwa na mtetea tu, nikishapata hukumu itabidi nikutane naye, nisikie maoni yake, niangalie sheria, mwenendo wa shauri, niangalie ni kitu gani ambacho mahakama ilijielekeza vibaya katika kufiakia uamuzi huo na kama itaonekana kipo tutaangalia hatua za kuchukua,” 
ni kauli iliyotolewa na wakili huyo siku hukumu ilipotoka.

Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaimaBlog leo ofisini kwake msajili wa mahakama kuu ya Tanzania Iringa Ruth Massam alithibitisha kupokea rufaa hiyo iliyowasilishwa na wakili Lwezaula Kaijage ambae ndie alikuwa akimtetea askari Simon .
"Ni kweli nimepokea notisi ya rufaa ya kesi hiyo ninayo hapa tokaJulay 29 mwaka huu ndipo ilipoletwa na kupokelewa mezani kwangu ....na taratibu nyingine zinaendelea "
Alisema msajili huyo kuwa kwa sasa anaendelea na taratibu za kimahakama ikiwa ni pamoja na kuijulisha mahakama kuu ya rufani Tanzania idadi ya rufaa ambazo ofisi yake imezipokea pia kuanza kuandaa taratibu nyingine zitakazowezesha mahakama kuu ya rufani Tanzania kutaja tarehe ya kusikilizwa kwa rufaa hiyo na nyingine .

Endelea kusoma habari hii kwenye chanzo cha taarifa, blogu ya MatukioDaima