Daktari wa Kongwa asimamishwa kazi kwa ulevi

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi amewasimisha kazi daktari mmoja na matabibu wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa tuhuma za uzembe na ulevi, limeripoti gazeti la MWANANCHI.

Akizungumza na uongozi wa Mji Mdogo wa Kibaigwa, Ndejembi alisema alikwenda katika hospitali hiyo ya wilaya usiku akakaribishwa na runinga iliyokuwa inawaka.
“Nilikaa pale kwa muda wa dakika 45 ndio akatokea mtumishi akasema kuwa alikuwa katika wodi ya watoto. Lakini unajua tu ipo shida,”alisema.
Alisema kesho yake aliitisha kikao na maazimio yakawa kwamba daktari hayo asimamishwe kazi wakati uchunguzi ukiendelea.

Aliwataja waliosimamishwa ni daktari wa Meno, Dk Waziri Majuto ambaye amesimamishwa kwa ulevi na matabibu wawili Daniel Ndahani ambaye alisimamishwa kwa kukosa weledi wa kazi na Denis Msovero hakuwepo kazini wakati alipoenda katika hospitali hiyo.