Huu uharibifu wa vifaa vya taka katika vituo vya mabasi yaendayo haraka vipi?

Hapa upande wa kulia ukionekana kuwa kifaa cha kuhifadhia taka kilisha chomolewa na kubakiza mfuniko tuu na papo hivi kwa zaidi ya mwezi sasa.
Ikiwa ni miezi michache kupita tangu mabasi ya mwendo wa haraka yaanze kufanya kazi kwa ufanisi mzuri, kumekuwa na mambo kadha wa kadha yanayoendelea ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya vituo hivyo vya mabasi hayo.

Hili limeonekana Morogoro Road ambapo kipande cha kutokea Jangwani mpaka Manzese kikionesha wazi vifaa vya kuhifadhia taka vimeharibika, huku vingine vikionekana kuchomolewa, kupinda, na kulegea.

Swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwa jinsi miundombinu hii ilivyo kaa ni ngumu sana hata mtu kugonga kwa mguu sasa inakuwaje inaharibika kiasi hiki?


Hapa Kifaa cha kuhifadhia taka taka kikiwa kimepinda haijulikani kiligongwa au kuna watu walikuwa wanataka chomoa.


Hiki kikiwa kimelegea kabisa amambapo muda wowote litachomoka


Hapa mfuniko ndio ulisha potea tena


Hili nalo tayari linaelekea kudondoshwa chini


Hii hapa ndio funga kazi kabisa yani wamesha chomoa muundo mbinu wote wa kushoto

  • Picha na Fredy Njeje