Karibu nyumbani Simbu na pongezi kwa kutuwakilisha vyema Rio Olympics 2016Mwanariadha Mtanzania wa mbio ndefu, Alphonce Felix Simbu (24) jana amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam akitokea nchini Brazil kwenye michuano ya Kimataifa ya Olimpiki.

Simbu alitia fora kwa kushika nafasi ya 5 kwenye siku ya mwisho ya michuano ya Olimpiki katika mashindano ya marathon jijini Rio de Janeiro nchini Brazil kwa kutumia saa 2:11:15.