Kila Mtanzania atakiwa kupima ardhi yake

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemtaka kila Mtanzania kuhakikisha anapima ardhi yake anayoimiliki ili aweze kupewa hati na Serikali.

Akihojiwa katika televisheni ya Clouds, Lukuvi alisema sehemu kubwa ya Tanzania haipo katika mipango hivyo wanachokwenda nacho sasa ni kuipanga, kuipima na kuirasimisha.
“Mwaka 2016, kila Mtanzania mwenye ardhi ahakikishe anatafuta mpimaji wa ardhi aipime ardhi yake ili awe na hati,“ alisema Lukuvi.